Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

WADAU ARUSHA WALIMLILIA MAREHEMU WILLY

NA GLADNESS MUSHI   WA FULLSHANGWE-ARUSHA
 
JIJI la Arusha ni moja ya mji ambao umepokea kwa masikitiko makubwa
kifo cha aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la jambo leo marehemu Willy
Edward (38) aliyefariki usiku wa juni 16 ghafla kwa kusababishwa na
mshutuko wa moyo.

Kifo hiki kimesitisha wadau mbali mbali wa mtandao huu ambao walikuwa
wapenzi watembeleaji  na pia hata wawakilishi wa mtandao huu kwa kuwa
kifo hicho kimetokea ghafla kwani amefariki dunia akiwa bado kijana
angali anahitajika kutoa mchango wake katika tasnia nzima ya
uahandishi wa habari.

Wakielezea kwa nyakati tofauti baadhi ya wadau mbali mbali mkoani hapa
wa jambo leo Bw. Adamu Aly alieleza kuwa kamwe hataweza kumsahau
marehemu kwa mchango wake katika tasnia ya habari kwa kuwa alikuwa
kijana mwadilifu na aliyekuwa anafanya kazi yake kwa umahiri ambapo
alikuwa hata ameipa tasnia ya uhabari sifa mbali mbali kutokana na
mawazo aliyokuwa akiyatoa.

“Marehemu Willy ni mmoja wa wahariri ambao alifanya kazi yake kwa
umakini ambapo kwa kweli inasikitisha sana kwani nimepokea msiba huu
kwa mshutuko mkubwa na huzuni nyingi kwani alikuwa kijana na bado
alikuwa anahitajika sana hasa katika kuendelea na umahiri wake wa
kazi lakini basi tu kazi ya Mungu haina makosa”alisema Adamu

Nae Qeen Lema mwandishi wa habari aliyefanya kazi na marehemu kwa
kipindi akiwa majira jioni akielezea kwa undani alivyomfahamu marehemu
alisema kuwa hatua aliyo kwa sasa amefika ni kwa ajili ya mhariri
huyo makini ambaye kila mara alikuwa akimpa
changamoto na miongozo mbalimbali kwa ajili ya kuweza kusonga mbele
zaidi kiuhandishi

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...