Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

TWIGA STARS YAPIGWA 1-0 NA ETHIOPIA UWANJA WA TAIFA

Mchezaji wa timu ya Twiga Stars Mawanahamisi Omary akiondoka na mpira kuelekea goli la timu ya wanawake ya Ethiopia huku mabeki wa timu hiyo wakiwania mpira huo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka ujao, mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Dar es salaam jioni hii.
Marefa wakiongoza timu za Ethiopia na Twiga Stars wakati zikiingia uwanjani tayari kwa mchezo huo jioni hii.
Wachezaji wa timu za wanawake wa Tanzania na Ethiopia wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa Twiga Stars na Ethiopia wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa.
Mpira umekwisha ambapo Twiga Stars imefungwa goli moja kwa bila na timu ya wanawake ya Ethiopia na kuwasukumiza nje ya mashindano hayo , Timu ya wanawake ya Ethiopia ilikuwa ikifanya mashabulizi mengi na ya nguvu katika lango la Twiga Stars kwa muda mrefu na dalili zilionyesha kwamba wataweza kupata goli pamoja na kwamba walikuwa wakicheza ugenini.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blogu

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...