AFANDE SELE HAMJUI NEY, AMFANANISHA NA NEEMA
"Simjui huyo Ney ni nani anaigiza filamu au ni demu gani? mimi najua majina kama hayo ni ya mademu sasa iweje Neema anidiss mimi?"
NI kauli ya nyota mwenye 'Crown' ya mkali wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele' alipokuwa akizungumza na Teentz.com kuhusiana na 'diss' dhidi yake iliyotolewa na msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuchana hivi sasa hapa Bongo, Ney wa Mitego kupitia track yake mpya iliyopewa jina la 'Nasema Nao'.
Akizungumza na mtandao huu namba moja ka habari za mastaa, Afande Sele mwenye maskani yake pande za Morogoro amesema kuwa kamwe hajawahi kusikia wala kujua kama kuna msanii wa hip hop hapa Bongo anayeitwa Ney na kusisisitiza kuwa hamjui huyo mtu kabisa.

Alipotakiwa kusema kama ameisikia Track hiyo Sele alifunguka kuwa hajui kitu chochote kuhusu wimbo huo na anaamini kuwa hakuna wimbo wa Hip hop ulitolewa hivi karibuni.
"Binafsi sijaisikia na sijui lolote,nitajaribu kufuatilia,nitaitafuta track hiyo niisikilize na kama atakuwa amefanya hivyo basi nitamlinganisha na mtu anayemtukana Usain Bolt halafu akaanza kukimbia alisema Sele.
No comments:
Post a Comment