Muanzilishi na mmiliki wa studio ya Cash Money, mjasiriamali
na rapa Brayan Williams(45) ‘BirdMan’ amemzawadia mwanamuziki wa
R&B, Justin Bieber gari ya kifahari aina ya ‘Bugatti Veyron’ yenye
thamani ya dola za kimarekani milioni 2 alilokuwa akitumia hapo awali.
“Uncle Stunna luv. My first Bugatti ♛ #generosity,” aliandika
Justin Bieber kwenye ukurasa wake wa Instagram sambamba na kuweka picha
ya mkoko huo wa bei chafu.
Katika picha ni gari aina ya Bugatti aliloposti Justin Bieber Instagram baada ya kupewa kama zawadi na Birdman.
Kwa wale wafuatiliaji ni kwamba, gari alilopewa Justin
Bieber ndio alilolitumia BirdMan kwenye video ya wimbo wake wa ‘Fire
Flame’ iliyotoka mwaka 2010. unaweza ukautazama mkoko huo wa bei mbaya
hapo chini.
No comments:
Post a Comment