TIMU
ya Manchester United imeendelea kusuasua katika Ligi Kuu ya England
baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Stoke City leo ikiwa ni
mechi ya nane kupokea vipigo katika ligi hiyo.
Mabao
yote ya Stoke yamefungwa na Charlie Adam katika dakika ya 38 na 52
wakati bao la Manchester United likifungwa na Robin van Persie dakika ya
47. Kwa matokeo ya leo, Man Utd imebaki na pointi zake 40.
Katika
mechi ya leo, wachezaji wawili wa Man Utd, Jonny Evans na Phil Jones
waliumia ambapo Jones alikimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi baada ya
kugongana na Jon Walters wa Stoke.
No comments:
Post a Comment