Fast Jet: Imetukomboa, Sasa tunaweza kutumia usafiri wa anga kwa bei nafuu
Pamoja na kuwa
ni muda mfupi sana tangu ilipoanza kufanya kazi nchini Tanzania lakini
ndani ya kipindi hicho kifupi, imeweza kuondoa ile dhana kuwa usafiri
wa ndege ni kwa ajili ya watu wenye vipato vya juu.
Faraja Temu
ambaye alisafiri na ndege hiyo akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro (Kia), akielekea Zanzibar, alimweleza mwandishi wa habari
kuwa “Sasa naweza kupanda ndege, Fast Jet wamerahisha sana maisha ya
usafiri.
“Ukiangalia bei
ambayo nimelipa, haitofautiani sana na gharama za kawaida za usafiri wa
mabasi. Naamini kwamba hivi sasa kila anayesafiri kwa basi, anaweza
kupanda ndege na ikawa nafuu zaidi kupitia Fast Jet.” Anachokizungumza
Ritha Kabese ni kweli kabisa, kwani mapinduzi ya sasa ya Fast Jet,
yanafanya usafiri wa ndege kuwa gharama nafuu mno na kusaidia watu wengi
zaidi katika usafiri wa anga Mathalan; kwa
usafiri wa basi kwenda Mwanza, nauli ni kati ya shilingi 45,000 mpaka
60,000. Fast Jet yenyewe inatoza nauli ya chini kabisa shilingi 43,000,
yaani usafiri shilingi 32,000 na kodi shilingi 11,000, jumla shilingi
43,000.
Vilevile
unapopanda Fast Jet, haikulazimu kuingia gharama za ziada kwa ajili ya
matumizi ya njiani. Kati ya dakika 45 na 60, unakuwa umeshafika
unapokwenda. Hakuna sababu ya
kutumia saa nyingi njiani au wakati mwingine kupitisha zaidi ya siku
ukisafiri, eti kwa kukimbia gharama za kusafiri kwa ndege, wakati Fast
Jet inakusafirisha kwa bei nafuu kuliko hata ile ambayo ungelipa kwa
basi.
No comments:
Post a Comment