TANZANIA yazoa tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika

Akitangaza matokeo hayo jana mjini
hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk. Phillip Imler wa
Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema sababu iliyopelekea
Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na vivutio vya
kipekee.
Akielezea
hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee
iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama
wanaohama kwa msimu maarufu kama annul animal migration.

Alisema kutokana na sifa ambayo
Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu itaendelea kuvitunza
kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na kuongeza pato la taifa.
“Afrika ina vivutio vingi vyenye
kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie rasilimali hizo kwa kuvitunza
na kuviendeleza,”alisema
“Kwa Tanzania ni bahati ya pekee
kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika ambazo ni za
Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na hifadhi ya Taifa ya
Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea kuwa iwapo watanzania
wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio vilivyopo nchini, nchi
itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye Mkurugenzi wa Hifadhi za
Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima Kilimanjaro ni mlima
mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya kushinda na watanzania
waendelee kuutunza.
Dkt Kijazi alisema kuwa hifadhi
hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa kila aina kama Big Seven,
Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na Mamba.

Aidha Waziri wa Maliasili na
Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi huo ni historia kubwa
duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
No comments:
Post a Comment