SERIKALI YAPATA MWEKEZAJI WA KUENDELEZA SEKTA YA KOROSHO HAPA NCHINI
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza (kushoto),akiongoza mkutano huo.
Kulia ni mdau wa zao la korosho.
|
Wadau wa sekta ya korosho wakiwa kwenye mkutano huo |
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza. (kushoto), akiongoza mkutano
wa uendelezaji wa sekta
ya korosho.wengine ni wadau wa zao hilo.
|
Wadau wa kilimo wakiwa katika mkutano wa uendelezaji
wa sekta ya korosho.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema imempta mwekezaji kutoka nchini Uingereza ambaye ameonesha nia ya kuja kuwekeza katika sekta ya korosho hapa nchini.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza alisema mwekezaji huyo yupo nchini kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.
"Kuna mwekezaji ambaye yupo nchini akikamilisha mchakato wa kuendeleza sekta ya korosho na tayari tumefanya naye mazungumzo kwa awamu mbili" alisema Chiza.
Alisema mwekezaji huyo anaangalia namna ya kujenga viwanda vya kubangua korosho na kusindika na kuwa lengo lake ni kuwainua wakulima kupitia zao hilo na yeye mwenyewe kupata faida.
Chiza alisema Wizara ya Kilimo na Chakula wamekwisha fanya mazungumzo na mwekezaji huyo na juzi walikuwa naye wakikamilisha mchakati huo kwa kuwahusisha wakuu wa mikoa minne ya Pwani na Ruvuma pamoja na wadau wa zao hilo.
Alisema mwekezaji huyo anazungumza na wamiliki wa viwanda mbalimbali vya korosho ili kuona ni jinsi gani atafanya nao kazi.
Chiza alisema kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto katika uuzaji wa zao hilo kupitia vyama vya ushirika ambapo ulisababisha tani 65 za zao hilo kushindwa kuuzwa na kubaki kwenye maghala.
"Viongozi wa vyama vya ushirika ambao hawakuwa waaminifu ndio waliosababisha kutokea kwa changamoto hiyo baada ya kukopa fedha katika mabenki na kushindwa kununua zao hilo'' alisema Chiza.
Alisema hapa nchini kuna viwanda vya kubangua korosho 12 vinavyo milikiwa na wazawa lakini kinachoendelea na kazi ni kimoja tu hivyo serikali imejipanga kuvikopesha ili viweze kufanya kazi na kupunguza changamoto ya korosho kuuzwa kwa bei ya chini.
Aliongeza kuwa pamoja na kuvifufua viwanda hivyo wanampango wa kubadilisha sheria ya korosho ya mwaka 2003 ili wapate mpya ambayo itakuwa na meno zaidi ya kuwabana walanguzi wa zao hilo.
Chiza hakuwa tayari kutaja jina la mwekezaji huyo kwa madai ni mapema kibiashara kwani wanaweza kuibuka watu wengine na kuharibu mchakato huo.
No comments:
Post a Comment