Waziri Mkuu alikuwa akutane na
Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa
Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha
wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho. Kwa
sasa anakula chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara
kitafuatia. Kutokana na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya siasa ya CCM mkoa,
wabashiri wengi wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano
mkali.
Dondoo Muhimu
*Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa
bomba la gesi kwenda Dar.
*Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka
Waziri Mkuu aondoke naye.
*Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa
kauli moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka yake kutoa kauli
za uongo kuhusu Mtwara vijijini kuunga mkono suala la gesi kusafirishwa kwenda
Dar, Madiwani wa Mtwara vijijini wamesema
hawakushirikishwa.
*Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani
na Mkuu wa Wilaya
*Waziri Mkuu kutumia mbinu ya
kisiasa kuwashawishi bomba liende Dar
*Wajumbe wameondoka kwa shingo
upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu.
*Kikao kinafanyika chini ya ulinzi
Mkali wa FFU, JWTZ na Usalama wa Taifa.
*Hawa Ghasia arudishwa uwanja wa
Ndege JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya
hewa.
*Polisi wanadai Meya anataka
kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio
chanzo cha vurugu
|
No comments:
Post a Comment