VIDEO YA NEY NUSURA IMTOE ROHO
Staa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, anayemiliki jina la Ney wa Mitego amenusurika 'kudanja' kufuatia mlipuko mkubwa wa moto wakati alipokuwa akikamilisha zoezi la upigwaji picha (shooting) za video za wimbo wake mpya uliopewa jina la Nasema nao ambao ndani ametoa diss kibao kwa wasanii kadhaa wa muziki huo.
Akizungumza na Teentz.com muda mfupi uliopita Ney ambaye sasa amejipachika jina la 'True Boy' amesema kuwa kulikuwa na matukio mengi ya kushangaza wakati kuanza kwa zoezi la kuchukua video hiyo ikiwemo watu kuungua moto na wengine kukatwa na mabati wakati wa harakati hizo.
No comments:
Post a Comment