Taarifa ya Utekelezaji wa National Sanitation Campaign (NSC) Upande wa Wizara ya Maji, Kwenye Hafla ya Kusainiwa Participation Agreement ya NSC
Mhandisi Bashiri Mrindoko Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya wizara hiyo Ubungo maji wakati wizara nne zilipotiliana sahihi maafikiano ya utekelezaji wa Participation Agreement ya NSC, Programu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP). Programu hii ndogo inafadhiliwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo na kutekelezwa na Halmashauri zote hapa nchini , Wizara zinazohusika na mkataba huo ni Wizara ya Maji na Umwagiliaji, TAMISEMI, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
Mhandisi Bashiri Mrindoko Naibu Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji wa pili kutoka (kushoto)akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya utekelezaji huo, wanaosaini kutoka kulia ni Elias Chinamo Mkurugenzi Msaidizi Mazingira, Afya na Maji Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Aelestin GesimbaKaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi na kushoto ni Winfrida Nshangeli Mkurugenzi Uratibu wa Sekta TAMISEMI
1.0 Utangulizi
Wizara ya Maji ikishirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza Programu ndogo ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji(WSDP). Programu hii ndogo inafadhiliwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo na kutekelezwa na Halmashauri zote hapa nchini zipatazo 132.
Programu hii, ilianza kutekelezwa mwaka 2006. Wakati huo kazi zote zilisimamiwa na Wizara ya Maji. Kazi hizo zilijumuisha utafutaji wa fedha, ujenzi wa miradi mipya na ukarabati wa miradi ya zamani ya maji. Kazi zingine zilikuwa ni uhamasishaji wa Usafi wa Mazingira majumbani na mashuleni.
Mwaka 2010 Wizara ya Maji na Washirika wa Maendeleo walifanya mapitio ya uendeshaji wa WSDP. Moja ya makubaliano katika mapitio hayo ilikuwa majukumu ya utekelezaji wa kazi za usafi wa mazingira yatekelezwe chini ya usimamizi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati Wizara ya Maji ikibaki na jukumu la kutafuta fedha na kufanya uratibu wa utekelezaji. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) zinakuwa na jukumu la utekelezaji kwa upande wa mashuleni na Wilayani sawia.
Fedha za utekelezaji wa Usafi wa Mazingira Vijijini kwa muda wa miaka minne imekadiriwa kuwa dola za kimerekani milioni 20 ambazo sawa na shilingi billioni 30 fedha za kitanzania. Kati ya fedha hizo kiasi cha dola za kimarekani 4.75 milioni ambazo sawa na shilingi bilioni 7.125 fedha za kitanzania zitatolewa na kutumika katika mwaka wa fedha wa 2012/2013.
Dhumuni kuu la Usafi wa Mazingira Vijijini ni kuboresha Usafi wa Mazingira Majumbani na Mashuleni kupitia mbinu mbalimbali za kuhamasisha jamii juu ya usafi wa mazingira.
Utekelezaji wa mpango huu ndani ya miaka minne umelenga kushawishi kaya 1,300,000 kujenga na kutumia vyoo vilivyo bora. Aidha, jumla ya shule 700 zitafaidika na mpango huo kwa kuwa na vyoo, miondo mbinu ya maji safi na salama na miundo mbinu ya kunawia mikono baada ya matumizi ya choo.
No comments:
Post a Comment