Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

WAZIRI WA HABARI, DKT. FENELLA AMTEUA DKT. SEWANGI KUWA KATIBU MTENDAJI BAKITA


Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, amemteua Dkt. Selemani Sewangi (55) kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa  (BAKITA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa wizara  hiyo, uteuzi huo umeaanza rasmi  Julai Mosi mwaka huu.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Dkt. Sewangi  ni Mhadhiri Mwandamizi wa Taasisi za Kiswahili (TATAKI) kutoka  Chuo Kikuu cha Dares Salaam.

Dkt. Sewangi anachukua nafasi hiyo iliyoachwa na Dkt. Anna Kishe, aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...