Waziri Haroun Ali Suleiman azindua mradi wa kupunguza umasikini miongoni mwa watoto na vijana
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Haroun Ali Suleiman ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Áfrika( ADB) kwa kuweza kuendeleza mradi wa elimu mbadala na amali kwa awamu ya pili.
Akitoa shukrani hizo leo huko katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzíbar wakati akizindua mradi huo wa awamu ya pili ambao umelenga kupunguza umasikini miongoni mwa watoto na vijana ambao hawakuweza kumaliza masomo yao ya skuli na wale ambao hawakubahatika kupata elimu kabisa .
Jumla ya sh million 23 dola za kimarekani zimetolewa na Benki hiyo kwa ajili ya kuendeleza mradi wa elimu mbadala na amali .
Waziri huyo alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuwapa uwezo vijana wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu pamoja na kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujuzi ambao utawasaidia kimaisha .
Aidha alieleza kuwa pamoja na juhudi hizo za wafadhili kazi iliyopo hivi sasa ni kutoa mashirikiano ya pamoja kwa wale wadau wa kubwa wa Wizara tatu tofauti
Akizitaja Wizara hizo ambazo ni wadau wa elimu mjumuisho ni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ,Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo pamoja na Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika .
“Kazi iliyokuwepo mbele yetu ni kubwa sana anahitaji mashirikiano kwa umoja wetu” alisema Haroun.
No comments:
Post a Comment