Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

SAMAHANI KWA PICHA HIZI!!!!!

MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST.AGREY MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI

Samahani kwa picha hizi



Hii ndiyo pikipiki inayodaiwa mwanachuo huyo kuiiba

Hiki ni kitambulisho cha mwana chuo huyo



Mwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey kilichopo uyole jijini mbeya anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba pikipiki zakusafirishia abiria maarufu kama bodaboda.


Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa kuwa na umri kati 25 mpaka 30 .


Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo july 2 mwaka huu majira ya saa 8 za mchana katika daraja lilopo karibu na hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea isanga jijini mbeya.


Amesema mtuhumiwa amekumbwa na mkasa huo baada yakupewa taarifa za kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina T-BETTER yenye alama ya chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya JOSEPH KAPASI(23)mkazi wa Ilomba jijini hapa


 

Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo JOSEPH KAPASI amesema aliombwa kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae alipoanza kuendesha vizuri alitokomea nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la isanga akielekea barabara ya chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na wanainchi wenye hasira kali nakuanza kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...