Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

NGOZI NA KAZI YANGU VINANIPA DILI...


MSANII na mtayarishaji wa filamu za Swahiliwood, Aunty Ezekiel, amesema kuwa matokeo ya kuilinda ngozi yake kwa kutotumia ovyo vipodozi, yamekuwa na faida kubwa kwake.

Anasema kwa umakini huo, ngozi yake ina mwonekano wa kuvutia hivyo kumpa nafasi kubwa ya kupata kazi katika tasnia hiyo.

"Katika maisha yangu, ngozi ina thamani kubwa. Huwa nailinda isidhurike na kemikali, vipodozi vyangu ni vya kawaida kabisa," alisema baada ya kuchaguliwa kuwa balozi wa ZUKU.

"Situmii kemikali kabisa na sina gharama kama wengine, najivunia mwonekano wangu wenye kuvutia pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza, ndiyo maana nawashika wapenzi wa filamu.
"
Msanii huyo pamoja na Jacob Stephen walichaguliwa kuwa mabalozi wa Zuku Swahili Movie inayotarajia kuzinduliwa mwezi ujao.

Kwa ubalozi huo, wanatarajiwa kupata mikataba ya matangazo itakayohusu bidhaa za kampuni hiyo pia kushiriki katika kampeni mbalimbali za filamu

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...