Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akitoa maelezo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA Tanzania, uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar eSalaam Juni 15 2012, Uzinduzi rasmi umefanywa na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete. Mradi wa Fistula kwa mwaka inakadiriwa wastani wanawake wapya 2,500 hadi 3000 hupatwa na ugojwa huo wakati wanapojifungua. Kwa sasa wanawake zaidi ya 31,000 inasemekana wanalo tatizo la Fistula hapa nchini, Hivyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito wakina mama wenye matatizo ya Fistula kumuacha kujificha kwani unatibika .hivyo waende katika matibabu ambayo hupatikana bure ktk hosp. ya CCBRT jijini DSM na hosp, ya Kilutheli ya Selian. (Picha Zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO). |
No comments:
Post a Comment