TASWIRA ZA MBUNGE WA JIMBO LA UBUNGO JOHN MNYIKA MARA BAADA YA KUSHINDA KESI YA UBUNGE DHIDI YAKE LEO
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh.John Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. John Mnyika akiwa amebebwa juu juu na Wanachana wa Chama hicho pamoja na washabiki wake nje ya Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo mara baada ya kushinda kesi yake iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na Ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Wanachama wa Chadema pamoja na washabiki wa Mbunge wa Jimbo la Ubungo wakishangilia ushindi wa kesi ya Mbunge wao,Mh. John Mnyika
Mnyika akipongezwa na Baadhi ya jamaa zake waliofika Mahakamani hapo.
Askari Polisi wakihakikisha usalama upo wa kutosha katika njia walizokuwa wakipita wapenzi wa Chadema kusherehekea ushindi wa Mbunge wao.Mh. Mnyika alipokuwa akiwasili Mahakamani leo asubuhi.
Wafuasi na Wanachama Wa Chama Cha demokrasi na Maendeleo CHADEMA wakiwa kwenye maandamano katika barabara ya bibi titi mohamed kuelekea ubungo mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh John Mnyika Kuibuka Kidedea katika Kesi ya Ubunge wa Jimbo la Ubungo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge Jimbo hapo Bi Hawa Ng'umbi katika Uchaguzi Mkuu Uliofanyika Mwaka 2010.Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog na Fununu Habari
Yule Hausigeli Anayedaiwa kuua Mtoto wa Bosi Wake Huyu Hapa

Mfanyakazi wa ndani anayetuhumiwa kumuua mtoto wa mwenye nyumba katika eneo la Sinza Mori akiwa amewekwa chini ya ulinzi na majirani wa eneo hilo. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM, Gea Habib.Picha na Evance Ng’ingo
--
MSICHANA wa kazi za ndani anayetuhumiwa kumuua mtoto wa bosi wake, juzi usiku alinusurika kudhuriwa baada ya kukamatwa na bosi wake aliyejulikana kwa jina moja la Mama Angel.
msichana huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa), akikamatwa juzi saa 6 usiku Sinza nyumbani kwa Mama Angel. Baada ya kukamatwa, majirani wa Mama Angel ambao walishiriki msiba wa mtoto huyo, walishirikiana kutaka kumchukulia sheria mkononi.
Inadaiwa kuwa msichana huyo alisababisha kifo cha mtoto huyo wa miezi saba wakati Mama Angel akiwa kazini Machi mwaka huu na kutoroka nyumbani hapo.
Kijana wa mwenye nyumba hiyo, Ally Hasan alidai alikuwa wa kwanza kugundua kuwa mtoto huyo amekufa baada ya Mama Angel kumpigia akimuomba kumuangalizia mtoto wake huyo aliyekuwa amemuacha amelala. Kwa Habari Kamili
No comments:
Post a Comment