RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe uliowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Bwana, Sidney Sekeremayi, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Bwana Sidney Sekeremayi, ambaye ni mjumbe maalumu wa Rais Robert Mugabe Ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Picha na Freddy Maro
JANUARI MAKAMBA AFANYA ZIARA MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONI YA AIRTEL
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) akipokewa na Mkurugenzi Mtendai wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor, alipofanya ziara kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilino\ wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) akipokewa na Ofisa Mkuu wa Biashara wa Airtel Tanzania, Chiruwi Walingo alipokwenda kufanya ziara ili kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano Mallya akiongozana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kushoto) katika ofisi za makamo makuu ya Airtel wakati wa ziara yake kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sam Elangallor (katikati) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (kulia) na ujumbe wake wakati wa ziara ya naibu waziri huyo kukagua shughuli mbalimbali za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment