Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

KISUMA BAR YAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA SAFARI LAGER NYAMA CHOMA DAR 2012

Mchomaji nyama mkuu wa Jiko la Baa ya Kisuma, Temeke, Dar es Salaam, Jerome Kavishe akiwa amebebwa na wafanyakazi wa baa hiyo, baada jiko hilo kuibuka wa kwanza katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Alizawadiwa cheti na sh. mil 1,000,000 katika kilele kilichofanyika Jumapili kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni. Washindi wa pili ni Bar ya Fyatanga, ya Tatu Titanic, ya nne Meeda na wa mwisho ni Play Time. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
Mrema wa Kisuma Bar akiandaa ndafu wakati wa mashindano hayo
 Uchomaji nyama unaotakiwa
 Mshindi akionesha fedha na cheti , Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo wadhamini wa mashindano hayo
Furaha ya wafanyakazi wa Kisuma Bar baada ya kutangaziwa ushindi
 Ilikuwa ni cheleko cheleko kwa wafanyakazi wa Kisuma Bar

     Wafanyakazi wa Kisuma wakizidi kuonesha manjonjo
 Mmoja wa wafanyakazi wa Kisuma Bar, akicheza huku akiwa na nyama choma mkononi
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika fainali hizo
Nyama ikiandaliwa vizuri katika bar ya Meeda ambayo ilishika nafasi ya nne katika mashindano hayo
    Mambo ya Meeda
 Baadhi ya wakazi wa Jiji wakijichana nyama choma na kupata vinywa vinavyozalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
 Majaji wakionja nyama kabla ya kuamua mshindi ni nani. Kulia i ni Abdalah Wakulichombe na Lawrence Salvi
Nyama choma ya ng'ombe, mbuzi na kuku pamoja na kachumbari pembeni   
   Maandalizi ya nyama choma
    Akina dada wakisuburi nyama choma
  Jamani mnaona nyama inavyochomwa?
 Nyama choma ikiandaliwa katika banda la Bar ya Play Time, iliyoshika nafasi ya mwisho
    Sehemu ya watu waliofika kushuhudia mpambano huo
   Kila mchomaji nyama alikuwa bize kuhakikisha anashinda
    Ndizi zikiwa zimeandaliwa vizuri
 Muhidini Issa Michuzi hakukosa katika tukio hilo, kama anavyoonekana akiwinda kuwapiga picha mbuzi waliofika kushuhudia mashindano hayo ya nyama choma
   Mmoja wa washindi akifurahia kupata cheti na fedha
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Michezo Wilaya ya Kinondoni,Said Mbwecha akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi. Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

   Jamaa wakijichana nyama choma iliyoandaliwa vizuri

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...